Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmed
Davutuglo, anasema kuwa zaidi ya watu 15,000 wamekusanyika kwenye mpaka
wake, wakitoroka mashambulizi makali yanayoongozwa na Urusi, Kaskazini
Mashariki mwa Syria.
Waziri huyo Mkuu anaamini kuwa makumi ya maelfu ya wakimbizi wengine wako njiani kuelekea kwenye mpaka huo.
Hadi kufikia sasa wakimbizi hao hawaruhusiwi kuingia Uturuki.
Hata hivyo wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya Uturuki wameruhusiwa kuvuka mpaka na kutoa misaada kwa watu hao.
Wakimbizi
hao walitimuliwa makwao wakati wanajeshi wa Syria,wakiungwa mkono na
mashambulizi ya ndege za kijeshi za Urusi, walipotekeleza mashambulizi
katika mji wa Allepo.