Tetemeko kubwa la ardhi limekumba
Taiwan Kusini, na kuangusha jengo moja la ghorofa 17 ambapo hadi kufikia
sasa watu watatu wamethibitishwa kufariki.
Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi
ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali
wanajaribu kuwafikia
watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama
katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara
ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo
lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa
zaidi.