Urusi imesema kuwa imetekeleza
shambulio kali zaidi dhidi ya maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa
Islamic State nchini Syria,ikiwa ni miongoni mwa mashambulizi yake ya
hewani kufikia sasa.
Waziri wa ulinzi Sergei Shoigu,amethibitisha
ripoti za Ufaransa na Marekani kwamba Moscow ilitumia mabomu ya masafa
marefu na makombora .
Amesema kuwa ndege hiyo ilirusha makombora
katika maeneo ya wapiganaji hao mjini Raqqa,ambao ndio ngome kuu ya
wapiganaji hao na Deir ez Zor mashariki mwa Syria,huku mabomu yakilenga
Kaskazini.
Awali rais Vladmir Putin alionya mashambulizi makali
dhidi ya IS,kufuatia thibitisho kwamba ndege ya Urusi ilioanguka nchini
Misri mwezi uliopita ilisababishwa na shambulizi la kigaidi.
Maafisa wa Urusi wanasema kuwa chembechembe za vilipuzi zilionekana katika mabaki ya ndege hiyo aina Airbus.
Abiria wote 224 walioabiri ndege hiyo ,wengi wao wakiwa watalii wa Urusi waliuawa.
Kundi la Islamic State limethibitisha kutekeleza shambulio hilo.